Search

उपदेश

Somo la 11: Maskani

[11-21] Kuhani Mkuu Aliyetoa Sadaka ya Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:1-34)

Kuhani Mkuu Aliyetoa Sadaka ya Siku ya Upatanisho
(Mambo ya Walawi 16:1-34)
“BWANA akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni, walipokaribia mbele za BWANA, wakafa; BWANA akamwambia Musa, Sema na Haruni na ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema. Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ngo’ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini na kuyavaa. Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya BWANA, na kumtoa awe sadaka ya dhambi. Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za BWANA ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni amtasongeza ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, nakufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake. Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za BWANA, na konzi mbili za uvumba mvuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ngo’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba. Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo afanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ngo’ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema, naye afatanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao. Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. Kisha atatoka na kuiendea madhahabu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. Tena atainyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke. Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo; naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu na kuvaa nguo zake, na kutoka na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu. Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguzo zake na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago. Na yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachomwa moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao. Na yeye awachomaye moto atafua nguzo zake na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia maragoni. Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yoyote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu. Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA. Ni sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. Na kuhani atakayetiwa mafuta ya kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani yale mavazi matakatifu. Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko. Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile kama BWANA alivyomwamuru Musa.”
 

Kuhani Mkuu alikuwa ndiye aliyetoa sadaka ya Siku ya Upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli. Sadaka hii ilitolewa mara moja kwa mwaka katika siku ya kumi ya mwezi ya saba katika kalenda ya waisraeli. Katika siku hii, wakati Kuhani Mkuu Haruni alipokuwa akitoa sadaka kwa niaba ya watu wa Israeli kwa ajili yao, maovu yao yote yalipitishwa katika mwanasadaka huyu wa kuteketezwa na damu ya mwanasadaka huyu ilizisafishia mbali dhambi zao. Kwa hiyo Siku ya Upatanisho ilifanyika kuwa ni siku kuu kwa watu wa Israeli. 
Kama kwa sadaka nyingine, sadaka ya Siku ya Upatanisho pia ilipaswa kuandamana na mambo matatu yasiyobadilika: mnyama wa sadaka ya kuteketezwa asiye na mawaa, kuwekewa mikono, na kumwaga damu ya mwanasadaka wa kuteketezwa. Hivyo Mungu alipokea kwa raha sadaka zilizotolewa kwa namna hii. Tofauti ya sadaka hizi na sadaka nyingine ni kwamba Kuhani Mkuu alipaswa kuichukua damu kwenda nayo Patakatifu pa Patakatifu. 
Baada ya kutoa sadaka kwa ajili yake mwenyewe na kwa nyumba yake, Haruni Kuhani Mkuu alitoa mbuzi wawili kwa Mungu na kwa ajili ya watu wa Israeli. Kwanza, alimtoa mbuzi mmoja kwa ajili ya Bwana Mungu kwa mfano ule ule alivyotoa sadaka ya dhambi ya ng’ombe dume. Na kisha alitoa mbuzi wa pili kuwa mbuzi wa kisingizio. Alizipitisha dhambi za watu wa Israeli katika mbuzi huyu wa kisingizio kwa kuiwekwa mikono yake katika kichwa chake mbele ya waisraeli, na huyu mbuzi ambaye amezipokea dhambi zao alipelekwa jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 
 


Sadaka ya Siku ya Upatanisho Ilizisafishilia Mbali Dhambi Zote za Watu wa Israeli

 
Katika Siku ya Upatanisho, Kuhani Mkuu akiwawakilisha watu wa Israeli alizipitisha dhambi zao katika kichwa cha sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yake juu yake. Aliwaleta mbuzi wawili walio hai, akapiga kura juu yake—mmoja kwa ajili ya Mungu na mwingine kwa watu wa Israeli. 
Kule kuwekea mikono hapa kuna maanisha kuzipitisha dhambi zote katika sadaka ya kuteketezwa kwa kuweka mikono juu ya kichwa chake. Huku kuwekea mikono ilikuwa ni mbinu ya kuziosha dhambi iliyokuwa imepangwa na Mungu, na pia katika kipindi cha Agano Jipya mbinu hii katika muundo wa kuwekea mikono ilipaswa kutumika sawasawa kwa Yesu ili aweze kuzioshelea mbali dhambi zote za mwanadamu. Ili kuziondoa dhambi za Kuhani Mkuu mwenyewe, dhambi za nyumba yake, na dhambi za mwaka mzima za watu wa Israeli, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na kisha kuzipitisha dhambi zote juu yake. Kwa kuwa Kuhani Mkuu alikuwa amezipitisha dhambi za watu wa Israeli katika sadaka ya kuteketezwa kwa kule kuiwekea mikono juu ya kichwa chake, basi dhambi zote za mwaka mzima za waisraeli zilitoweshewa mbali. Vivyo hivyo, kwa kupitia sadaka ya Siku ya Upatanisho, watu wa Israeli waliweza kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa toka katika dhambi zao zote. 
Mtu yeyote aliye na dhambi amehukumiwa pasipo kukwepa. Kwa kuwa ili sadaka ya kuteketezwa iweze kuhukumiwa adhabu kwa haki kwa ajili ya dhambi za watu ilipaswa kwanza kuzipokea dhambi zao. Ikiwa Kuhani Mkuu angetoa sadaka kwa Mungu bila kuwekea mikono yake juu ya kichwa cha sadaka, basi sadaka hii ingekuwa ni dhihaka kwa Mungu na kwa hiyo angelipaswa kuacha kuitoa sadaka hiyo. Ili kuwaokoa wanadamu wote waliokuwa wameigeukia dhambi, Mungu alikuwa ameanzisha mpango wake wa wokovu uliotimizwa kwa kupitia mbinu za kuwekewa mikono. Ili kuzitoweshea mbali dhambi za watu wa Israeli, Mungu alimwinua Kuhani Mkuu na alimfanya kuzipitisha dhambi zote za watu wake mara moja na kwa wote kwa kuiweka mikono yake katika kichwa cha sadaka ya kuteketezwa kama mwakilishi wao. Kwa hiyo, wanyama wote wa kuteketezwa waliotolewa kwa Mungu katika Hema Takatifu la Kukutania walizipokea dhambi za waisraeli kwa kuwekewa mikono, kisha wakabeba adhabu ya dhambi kwa niaba yao na kuimwaga damu yao na kufa. 
Ili kuitimiza haki ya Mungu na upendo wa Mungu kikamilifu, waisraeli walipaswa kutoa sadaka ya Siku ya Upatanisho kwa Kuhani Mkuu kuiweka mikono yake juu ya sadaka ya wanyama wa kuteketezwa na kisha kuwachinja na kuimwaga damu yao kwa haki mara moja kwa mwaka. Kwa maneno mengine, kwa kupitia sadaka hii Mungu alipenda kuzioshelea mbali dhambi za mwaka mzima za watu wa Israeli mara moja na kwa wote. Hii ilikuwa ni sheria ya Mungu ya upendo ambayo ilizimitiza rehema zake na haki yake. Kwa kuwa Mungu ni mwenye haki, basi ili kuzitoweshea mbali dhambi zote za watu mara moja kwa mujibu wa sheria yake ya haki, Mungu alimwandaa Yesu Kristo Mwanakondoo na akamfanya kuzipokea dhambi katika mwili wake kwa kuwekewa mikono na kisha kuimwaga damu yake Msalabani. 
Yesu, ambaye alikuwa amejitoa yeye mwenyewe kama sadaka ya milele, alibeba dhambi za kila mtu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kupitia mbinu hii, alimwaga damu yake mara moja na kwa hiyo ameutimiza wokovu wao toka katika dhambi. Kwa hiyo, sisi pia ni lazima twende mbele za Mungu tukiwa na imani inayoamini katika ukweli wa wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa imani hii ndipo dhambi zote zinaweza kuondolewa mara moja na kwa wote. Kwa hiyo, yeyote anayependa kupokea ondoleo la dhambi zote mara moja ni lazima aje kwa Mungu akiwa na imani inayoamini kwa kweli katika injili ya maji na Roho. 
 


Maana ya Kuwekewa Mikono

 
Kuwekewa mikono kuna maanisha “kupitishiwa, kuhamishiwa, au kuzikwa” (Mambo ya Walawi 1:3-4). Wakati mtu yeyote wa kawaida alipotenda dhambi pasipo kukusudia na kisha akaitambua dhambi hiyo, basi alipaswa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu (Mambo ya Walawi 4:27-29). Kwanza alipaswa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa asiye na mawaa, kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mwanasadaka huyo kwa kuweka mikono juu ya kichwa chake. Kisha alipaswa kumchinja, kuikinga damu yake, na kisha kumpatia damu hii kuhani (Mambo ya Walawi 4:27-28). Kisha Kuhani aliichukua baadhi ya damu hii kwa kidole chake na kuiweka katika pembe ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kisha kuimwaga damu yote iliyosalia chini ya ile madhabahu. Pia alipaswa kuyachoma mafuta yake juu ya ile madhabahu, kisha Mungu aliinusa ile harufu nzuru ya kuungua kwa mafuta iliyotolewa toka katika sadaka hii. 
Tumekwisha kujifunza kuwa ili kuzitoweshea mbali dhambi za watu wa Israeli, Mungu aliitayarisha siku ya Sadaka ya Upatanisho ambapo mikono iliwekwa juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha damu yake ikakingwa. Kwa namna hii pia, Mungu asingelizioshelea mbali dhambi za waisraeli ikiwa pasipo kule kuweka mikono juu ya sadaka ya kuteketezwa. Vivyo hivyo, sadaka ya Siku ya Upatanisho ambayo ilitolewa katika Agano la Kale inahusiana kwa karibu na ubatizo na damu ya Yesu katika kipindi cha Agano Jipya. 
Kama ambavyo sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale ilivyopaswa kuwa ya mnyama asiye na mawaa, katika kipindi cha Agano Jipya, Yesu alikuja kama Mwanakondoo wa Mungu asiye na mawaa, alibatizwa na kuimwaga damu yake Msalabani ili kuyaoshelea mbali maovu yote ya wenye dhambi. Kama ambavyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa alivyopaswa kuyapokea maovu ya wenye dhambi kwa kuwekewa mikono katika Agano la Kale, basi dhambi zote za ulimwengu zilipitishwa kwa Yesu wakati Yohana Mbatizaji alipoiweka mikono yake katika kichwa cha Yesu ili kumbatiza katika Mto Yordani (Mathayo 3:15). Sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale na ile ya Yesu ya Agano Jipya zote zilipaswa kupokea kule kuwekewa mikono na kisha kutoa damu hadi kifo kwa njia ile ile. Sadaka ya kuwekea mikono na kuimwaga damu ilikuwa ni sadaka ile ile ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya wenye dhambi katika Agano la Kale na Agano Jipya kadhalika. 
 

Kwa Hakika Dhambi za Mwanadamu Zinafuatiwa na Hasira ya Mungu
 
Sisi tulikuwa ni wenye dhambi mbele za Mungu ambao hatukuweza kufanya lolote zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi zetu kama ambavyo ile sadaka ya dhambi ilivyopaswa kuuawa kwa ajili ya dhambi ambazo ilikuwa imezibeba. Tunapoichora picha ya sadaka hii ya kuteketezwa ikiwa inachinjwa katika vipande na kisha kuchomwa kwa moto juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, basi tunaweza kutambua kuwa kama vilevile sisi pia tulikuwa tumefungwa ili tuweze kuangamizwa mbele za Mungu lakini bado Bwana ametuokoa kwa kubatizwa na Yohana na kuimwaga damu yake. 
Kwa hiyo, wale ambao hawajazaliwa upya ni lazima wakiri wenyewe kuwa ni wenye dhambi wanaoikabili adhabu kali ya dhambi ya kutisha kwa ajili ya dhambi zao mbele za Mungu na kisha waamini katika ubatizo na damu ya Yesu kuwa ni wokovu wao. Ili kutuokoa toka katika dhambi badala ya kutuhukumu kwa ajili ya dhambi hizo, Mungu aliandaa sadaka ya wokovu, akazipitisha dhambi zetu juu ya sadaka hiyo ya milele, akamfanya mwanasadaka huyo kuimwaga damu yake, na kwa hiyo ameziondolea mbali dhambi zetu zote (Mambo ya Walawi 16:1-34; Warumi 8:3-4, Waebrania 10:10-12). Je, bado una dhambi katika moyo wako? Basi ni lazima kwanza ukiri mbele za Mungu kuwa wewe ni mwenye dhambi unayeikabili adhabu ya dhambi ya Mungu, na kisha ni lazima uamini kwamba Yesu Kristo, ambaye ni Mungu ameutimiza mpango wa wokovu wako ambao alikuwa ameupanga hata kabla ya misingi ya ulimwengu. 
Dhambi haiwezi kupatanishwa pasipo kulipa fidia kamilifu. Hii ndiyo sababu Mungu aliwapatia watu wa Israeli utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Katika utaratibu huu wa sadaka ya kuteketezwa ni sadaka tu iliyoambatana na kule kuwekewa mikono na kuimwaga damu ndiyo iliyokuwa ni sadaka ya kweli ya imani ambayo ingeweza kuzioshelea mbali dhambi za waisraeli. 
Ni lazima tumtolee Mungu sadaka hii ambayo imewekewa mikono na kisha kuimwaga damu kwa imani na kwa mujibu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa iliyoandikwa katika Maandiko. Bwana aliimwaga damu yake kwa sababu alikuwa amezibeba dhambi zetu kwa kupitia ubatizo wake, alibeba adhabu ya dhambi hizi kwa haki kwa niaba yetu na kwa hiyo alimezitoweshea mbali hizi dhambi zetu (Mathayo 3:15; Yohana 1:29; Isaya 53:1-7). Tunapoamini katika Neno la maji na Roho, na tunapoiweka mikono yetu juu ya Bwana ambaye amefanyika kuwa sadaka yetu ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zetu zote juu yake, basi tunaweza kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini kwamba Bwana aliyezichukua dhambi zetu katika mwili wake pia alibeba adhabu ya dhambi hizi kwa niaba yetu. Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho tunaweza kuzipitisha dhambi zetu zote juu ya Bwana ambaye amefanyika kuwa sadaka yetu ya kuteketezwa, na tunaweza kufa pamoja naye na kisha kuishi tena pamoja naye (Warumi 6:1-11, Wagalatia 3:27).
Mafundisho ya kiroho ambayo tunapaswa kuyatambua toka katika sadaka ya Siku ya Upatanisho ni, kwanza kabisa, ni kwamba tunapaswa kuzitambua dhambi zetu na adhabu ya dhambi zetu, na kwamba tunapaswa basi kutoa sadaka ya imani ambayo Mungu anataka kuipokea—ambayo ni lazima tuwe na imani katika Yesu ambaye ameutimiza wokovu wetu kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani. Ni lazima tuiweke mikono yetu juu ya kichwa cha Yesu kwa kuamini katika ubatizo wake. Kwa nini? Kwa sababu ni pale tu tutakapoilaza mikono yetu juu ya sadaka ya kuteketezwa kwa imani na kuikinga damu yake ndipo tunapoweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote. 
Vivyo hivyo, yeyote anayetaka kuondolewa dhambi zake mbele za Mungu ni lazima alipe fidia ya uhai, kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Kama wewe ni tajiri au maskini ni lazima kuwe na sadaka ya kuteketezwa ambayo inalipa mshahara wa dhambi za mtu na gharama ya upatanisho ya uhai. Ni mpaka hali iwe hivi ndipo mtu anapoweza kupokea ondoleo la dhambi kwa imani. 
 


Sadaka ya Upatanisho ya Agano la Kale

 
Hebu tugeukie Mambo ya Walawi 16:6-10: “Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya BWANA, na kumtoa awe sadaka ya dhambi. Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za BWANA ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.”
Ili kuwawezesha watu wa Israeli kupokea ondoleo la dhambi zao kwa imani, Kuhani Mkuu kwa niaba yao alitoa sadaka ambayo iliambatana na kuwekewa mikono na kuimwaga damu. Sasa, imani ya Wakristo wa siku hizi ikoje? Je, si imani ya kufikirika na isiyo na msingi ambapo wanaitarajia sadaka yao kuzipokea dhambi zao hata kabla ya kuzipitisha dhambi zao juu yake? Ikiwa imani yako si aina ya imani ambayo imezipitisha dhambi zako kwa Yesu Kristo kwa kuwekewa mikono, basi kwa hakika una tatizo hadi sasa. Ikiwa imani yako haiamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani basi imani hiyo haiwezi kuwa imani ya kweli. 
Sisi hatukuweza kufanya lolote zaidi ya kushindwa kuifuata Sheria mbele za Mungu na tulifanya aina zote za dhambi katika mwaka mzima uliopita. Kwa hiyo kama tungelikuwa tumeishi katika kipindi cha Agano la Kale, basi tungalipaswa kupokea ondoleo la dhambi zetu kwa kuamini katika sadaka ya dhambi ambayo Kuhani Mkuu angekuwa ameitoa kwa niaba yetu. Ili kutoa sadaka ya imani kwa Mungu ni lazima tukiri kwanza kuwa tumefungwa ili kuharibiwa kwa ajili ya dhambi zetu, na ni lazima tuamini katika kule kuwekea mikono ambako kunazipitisha dhambi zetu zote katika sadaka ya kuteketezwa ambayo Mungu aliiandaa kwa ajili yetu na kuimwaga damu ya sadaka hii. 
Kwa kuwa kuwekea mikono juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kuimwaga damu yake kulikuwa na nguvu ya wokovu, basi watu wa Agano la Kale waliweza kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kupitia sadaka hii ambayo Kuhani Mkuu aliitoa kwa mujibu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa uliokuwa umepangwa na Mungu. Kwa kuiweka mikono yake juu ya sadaka ya kuteketezwa, Kuhani Mkuu alizipitisha dhambi za watu wake za mwaka mzima juu ya mwanasadaka huyo, akamchinja na kuikinga damu yake na kisha akainyunyizia damu hii mbele ya kiti cha rehema na katika upande wake wa mashariki mara saba. Kwa kufanya hivyo, hakuacha kamwe kutoa sadaka sahihi kwa Mungu kila mwaka. Hivi ndivyo watu wa Israeli walivyoweza kupokea ondoleo kamilifu la dhambi katika siku hizo. 
Vivyo hivyo, kwa kupitia sadaka ya dhambi ambayo Kuhani Mkuu aliitoa, watu wa Israeli waliamini na kuthibitisha katika mioyo yao kwamba dhambi zao zote zimeondolewa. Kitu ambacho sadaka ya Siku ya Upatanisho ya Agano la Kale inachotuonyesha ni kwamba katika Agano Jipya, Yesu Kristo alizichukua katika mwili wake dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana na akamwaga damu yake Msalabani, na kwamba ni lazima tuamini katika huyu Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu na tupokee ondoleo la dhambi la milele kwa imani. Nafsi zote za ulimwengu huu ambazo mioyo yao inateseka na kuhangaika juu ya dhambi zao ni lazima zitambue kuwa zinaweza kupokea ondoleo la dhambi la milele kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, na ni lazima nafsi hizo ziamini hivyo katika mioyo yao. Vivyo hivyo, sadaka ya ondoleo la dhambi zote ilikwisha pangwa na Mungu hapo kabla kama alivyoahidi kuwa ataitimiza, na ahadi hii ya wokovu imedhihirishwa pia katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambazo zilitumika kama vifaa katika Hema Takatifu la Kukutania. 
 
 

Sadaka ya Siku ya Upatanisho Imetimizwa katika Hema Takatifu la Kukutania

 
Katika Siku ya Upatanisho, ili kuzishughulikia dhambi zote za watu wa Israeli, Kuhani Mkuu aliiweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa mbele ya waisraeli wote (Mambo ya Walawi 16:1-23). Ilikuwa ni muhimu sana kwake kuzipitisha dhambi zao juu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yake katika kichwa chake kwa niaba yao. Wakati Kuhani Mkuu Haruni alipotoa sadaka ya Siku ya Upatanisho ndani ya Hema Takatifu la Kukutania kwa ajili ya watu wa Israeli, hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuingia katika Hema Takatifu la Kukutania. Lilikuwa ni tukio lisilo la kawaida kwa sababu ilizoeleka kuwamo makuhani wengi katika ua wa Hema takatifu la Kukutania isipokuwa tu katika Siku ya Upatanisho. 
Kuhani Mkuu alizipitisha dhambi za watu wa Israeli juu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa chake, alichukua damu ya sadaka hii na kwenda nayo katika Patakatifu pa Patakatifu, na akainyunyizia kwa kidole chake katika kiti cha rehema kwa upande wa mashariki; na pia alinyunyizia mara saba mbele ya kiti cha rehema (Mambo ya Walawi 16:14). 
Kwa wakati huu, zile kengele za dhahabu zilizokuwa zimeunganishwa katika upindo wa joho la Kuhani Mkuu zilikuwa zinagonga, na kwa hiyo kila wakati aliponyunyizia damu mbele ya kiti cha rehema na katika upande wa mashariki, kengele zililia na watu wa Israeli waliokuwa wamesimama nje ya Hema Takatifu la Kukutania waliweza kusikia sauti ya zile kengele. Wakati waisraeli walipoisikia sauti hii ya kengele walitambua kuwa Kuhani Mkuu alikuwa akitoa sadaka kwa Mungu kwa niaba yao. Na baada ya kuwa wameisikia sauti ya kengele kwa mara saba zote walipumua kwa unafuu kwa kuwa walitambua kuwa utoaji wa sadaka ya Siku ya Upatanisho sasa ulikuwa umekwisha hali ukithibitisha ukamilifu wa sadaka ambayo imezisamehe dhambi zao za mwaka mzima. 
Baada ya hili, Kuhani Mkuu Haruni alitoka nje ya Hema Takatifu la Kukutania akamchukua mbuzi mwingine aliyekuwa amesalia kuwa sadaka nyingine, na akaitoa sadaka hii ya Siku ya Upatanisho mbele ya watu wa Israeli. Mungu aliwaamuru watu wa Israeli kutofanya chochote katika Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:20-21, 29). Kuhani Mkuu aliiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa ili kuyatimiza majukumu yake na kisha kuipeleka sadaka hiyo kwenda jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari, mambo haya yalifanyika huku kundi kubwa la waisraeli wakiwa wamekusanyika kuona utoaji wa sadaka hii nje ya Hema Takatifu la Kukutania. 
Katika Siku ya Upatanisho, Kuhani Mkuu alileta mbuzi mbele ya watu wa Isareli akaiweka mikono yake juu ya kichwa chake na kisha akayatubia maovu yote makosa ya wana wa Israeli na akayapitisha kwa yule mbuzi. “Bwana, ninatubu dhambi zote ambazo watu wa Israeli wamezifanya katika mwaka mzima uliopita. Tumeshindwa kuifuata Sheria kikamilifu, tumefanya dhambi nyingi zisizohesabika dhidi yako na dhidi yetu wenyewe, tumeshindwa kuishi maisha ambayo ulituamuru tuyaishi, na tumefanya yale ambayo ulituagiza tusiyafanye. Tumezivunja amri zako nyingi sana katika mwaka mzima uliopita. Tumedanganya. Tumeua. Tumefanya uzinifu. Tumeiba.” Vivyo hivyo, Kuhani Mkuu alizipitisha dhambi zote za watu wa Israeli katika yule mbuzi wa kuteketezwa kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa chake mbele wa uwepo wao, na kisha alimpeleka yule mbuzi jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, Mungu hakumruhusu yule mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa kuishi baada ya kuwa amezipokea dhambi za watu wa Israeli. Yule mbuzi wa kisingizio ambaye aliachwa jangwani alipaswa kuteseka hadi kufa katika jangwa kwa kuwa alikuwa ameyabeba maovu yote, mawaa, na makosa ya watu wa Israeli. Sasa, watu wote wa Israeli walianza kuifurahia Siku ya Hema Takatifu la Kukutania [sikukuu ya vibanda] (Mambo ya Walawi 23:34) kwa sababu walikuwa wamezitupa dhambi ambazo zilikuwa zimewafunga kwa mwaka mzima kwa kupitia sadaka ya Siku ya Upatanisho. 
Kule kuwekea mikono ni njia mbayo kwa hiyo dhambi za watu wote zinapitishwa kwenda katika sadaka ya kuteketezwa. Wakati Kuhani Mkuu alipoilaza mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa, basi dhambi zote za watu wa Israeli ambazo zilikuwa zimelundikana kwa mwaka mzima zilipitishwa kwa mwanasadaka huyo mara moja na kwa wote. Kila dhambi ya kila mwisraeli ilipitishwa mara moja juu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kule kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu. 
Je, dhambi zote za watu wa leo zinaweza kupitishwa kwa sadaka ya kuteketezwa kwa kuwekewa mikono kama ambavyo maovu ya watu wa Israeli yalivyopitishwa kwa kuwekea mikono kwa Kuhani Mkuu katika Agano la Kale? Ikiwa hili haliwezekani, basi kuna njia gani kwa watu wa siku hizi ili waweze kupokea ondoleo la dhambi zao? Ni nani anayezipitisha dhambi za watu wa siku hizi, na ni kwa vipi na kwa kupitia nani? Kwa kulinganishwa na utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ulioanzishwa na Mungu katika kipindi cha Agano la Kale, Yesu Kristo alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika kipindi cha Agano Jipya. Kama ambavyo dhambi za mwaka mzima zilivyopitishwa kwa mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa mara moja na kwa wote kwa kupitia sadaka ya Siku ya Upatanisho ambapo Kuhani Mkuu alimtoa kwa ajili ya watu wa Israeli, basi vivyo hivyo dhambi zetu zilipitishwa kwa Yesu Kristo ambaye alibatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni Kuhani Mkuu wa mwisho. Je, dhambi zote za watu wa siku hizi zipo wapi? Dhambi hizo zipo juu ya kichwa cha Yesu Kristo. 
Kama ambavyo mbuzi wa kisingizio alivyozipokea dhambi zote za watu wa Israeli kwa kupitia Kuhani Mkuu kwa kule kuwekewa mikono, Yesu alifanyika sadaka ya kuteketezwa ya ondoleo la dhambi la milele kwetu sisi sote ambao tunaishi katika kipindi hiki kilichopo. Yesu ambaye alifanyika mbuzi wetu wa kisingizio alijitoa mwenyewe kwa Mungu kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa maneno mengine, Yesu alibatizwa na Yohana na akajitoa yeye mwenyewe ili kusulubiwa kama ilivyokuwa katika Agano la Kale. Mungu alikuwa amepanga sadaka ya kuteketezwa kwa watu wa Israeli na alizipitisha dhambi zao juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na akamhukumu mnyama huyo kwa niaba yao. 
Yule mbuzi wa kisingizio ambaye alipelekwa jangwani hakuweza kuishi kwa kuwa hakukuwa na maji zaidi ya jua kali lililokuwa likiwaka sana katika mchanga wa jangwa. Vivyo hivyo, Yesu pia hakuweza kukwepa bali kusulubiwa, kwa kuwa alikuwa amekwisha zichukua dhambi za mwanadamu za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake. Kama ambavyo mbuzi wa kisingizio alivyoachwa katika jangwa lisilo na uhai, Yesu ambaye alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake pia alichukiwa na kudharauliwa na watu wengi. Ikiwa mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa aliongozwa kwenda jangwani na kisha kuachwa huko akiwa peke yake, katika nchi isiyo na uhai, je, mbuzi huyo hakuzunguka zunguka na hatimaye kufa kwa kiu? 
Kwa namna iyo hiyo, Yesu ambaye alikuwa amezipokea dhambi zetu alikataliwa na watu wengi, na alisulubiwa ili kubeba adhabu ya dhambi zetu, akamwaga damu yake na kisha kufa. Huu ulikuwa ni wokovu ambao Yesu Kristo aliutimiza ili kutupatia wokovu wake wa kweli katika injili ya maji na Roho. 
Watu wa Israeli waliuona mchakato wa upatanisho wa ondoleo la dhambi kwa macho yao na waliamini juu ya ukweli huu katika mioyo yao. Kama wao, sisi nasi, tunaweza sasa kupokea ondoleo la dhambi zetu kwa kuona, kwa kusikia, na kuamini katika kazi za haki za Yesu Kristo katika mioyo yetu. Hii inatueleza sisi kuwa Yesu Kristo atabatizwa na Yohana, atazibeba dhambi za ulimwengu, atasulubiwa, ataimwaga damu yake, kufa, na kisha kufufuka tena toka kwa wafu na kwamba tutaokolewa kwa kuona yote haya kwa macho yetu ya kiroho na kuamini mambo hayo katika mioyo yetu. 
Sadaka hii ya Siku ya Upatanisho itaendelea kuwepo kadri waisraeli wanavyoendelea kuwepo. Waisraeli wanaendelea kutoa sadaka ya Siku ya Upatanisho katika siku ya 10 ya mwezi wa saba katika kalenda yao kwa sababu Mungu aliwaambia wao kuwa, “Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka” (Mambo ya Walawi 16:34). Mungu aliwapatia rehema zake wana wa Israeli ili kwamba dhambi zao zote ziweze kuoshelewa mbali na ili pia waweze kukombolewa toka katika dhambi zao kwa kuwafanya watu wa Israeli kutoa sadaka ya Siku ya Upatanisho kama hivi. 
Vivyo hivyo, Mungu amewawezesha watu wa siku hizi pia kutambua kuwa Yesu alizibeba dhambi zao zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, kwa kusulubiwa, na kwa hiyo amekamilisha kikamilifu kule kuziosha dhambi. Yesu Kristo alizibeba dhambi za mwanadamu kwa ubatizo wake na amefanyika kuwa Kuhani Mkuu wa milele wa Mbinguni. Sasa, hakuna kitu chochote kinachobakia kwa ajili yetu ili kukifanya kwa ajili ya wokovu wetu bali tunachopaswa kukifanya ni kuamini tu katika ukweli huu. 
 

Sadaka ya Upatanisho Mkuu Ambayo Masihi Aliitoa kwa Mungu Baba kwa Mwili Wake
 
Kwa nini Mungu aliwaamuru wana wa Israeli kumtolea sadaka ya Siku ya Upatanisho? Alifanya hivi ili kwamba waweze kutazama mbele kwa imani yao katika siku ile wakati Mungu Baba atamtoa Mwanae Yesu Kristo kutoa upatanisho mkuu kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote kwa ubatizo wake na kuimwaga damu yake. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu Baba na Mwokozi wa wanadamu alikuja hapa duniani ili kuzitoweshea mbali dhambi zote za kila mtu, akatimiza kila kitu kwa upendo wa Mungu, na akaufunua wokovu kwa mwanadamu. Kwa kubatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake na kwa kuimwaga damu yake Msalabani, Yesu amezitoweshea mbali dhambi zote na maovu ya ulimwengu, alihukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa kweli. 
Mungu alimwita Musa na akampatia kwanza Sheria. Kisha akamwagiza kulijenga Hema Takatifu la Kukutania kwa vifaa kama nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa, na akampatia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Kwa kufanya hivyo, Mungu aliwawezesha watu wa Israeli kutambua umuhimu wa kuwekea mikono na kuimwaga damu, na badala yake akawaonyesha juu ya Yesu Kristo, ambaye ni mlango wa wokovu uliotabiriwa katika Hema Takatifu la Kukutania, kwamba atakuja hapa duniani, atazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, atasulubishwa na kuimwaga damu yake. Wokovu wa kusafishwa dhambi ambao Mungu ametupatia unadhihirishwa vizuri katika vifaa vilivyotumika katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. 
Miongoni mwa vifaa vilivyotumika kwa ajili ya mlango wa Hema Takatifu la Kukutania, basi maana inayobebwa katika zile nyuzi za bluu ni kuwa Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kubatizwa na Yohana; nyuzi za zambarau zinatuonyesha kuwa Yesu ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, kwa kuwa aliuumba ulimwengu; nyuzi za rangi nyekundu zinatueleza kuwa kwa sababu Yesu alikuwa amebatizwa, basi alibeba adhabu ya dhambi kwa ajili ya wenye dhambi wote kwa kuimwaga damu yake Msalabani; na kitani safi ya kusokotwa inaelezea kwa upana juu ya huduma hizi tatu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na Mungu ametoa ondoleo la dhambi kwa wale wanaoamini katika Neno lake. 
Sasa, watu wote ni lazima wajikumbushe tena na tena na waamini kuwa ukweli huu—ambao unaeleza kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi wao na amewasafishilia mbali dhambi zao zote kwa kubatizwa na Yohana na kuimwaga damu yake Msalabani—ukweli huu pia unadhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambazo zimetumika kama vifaa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kwamba ni lazima wapokee ondoleo la dhambi zao. Kwa kupitia Musa, Mungu alianzisha sheria ya wokovu, sheria ya ondoleo la dhambi kwa wanadamu, na wakati ulipowadia, Mungu alimtuma Yesu Kristo kuja hapa duniani na akamfanya abatizwe na Yohana na kuimwaga damu yake Msalabani ili kwamba Yesu afanyike kuwa sadaka ya kuteketezwa ambayo itazioshelea mbali dhambi za ulimwengu. Na kwa kufanya hivyo, Mungu amewawezesha wote wanaoamini kuoshwa dhambi zao zote kwa imani. 
Kwa hiyo tunapokiri kuwa tunamwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu, basi ni lazima tuamini kwa kuufahamu ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake Msalabani. Kama ambavyo sadaka ya kuteketezwa katika Agano la Kale ilivyoyapokea maovu ya wenye dhambi kwa kuwekewa mikono na ilivyohukumiwa kwa haki kwa kuimwaga damu yake kwa niaba yao, Yesu Kristo alikuja kama sadaka ya kuteketezwa ya dhambi kwa ajili ya kila mtu anayeishi hapa duniani, alizichukua dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa, alisulubiwa na akaimwaga damu yake ya thamani, na kwa hiyo amezitoweshea mbali dhambi zetu mara moja na kwa wote, dhambi za wote wanaoamini. 
Ni lazima tuamini katika ukweli wa Neno la Mungu lililoandikwa kama lilivyo. Ukweli wa kibiblia ni kuwa kwa mbinu ile ile kama sadaka ambayo Kuhani Mkuu aliitoa kwa watu wake katika Agano la Kale, Yesu alikuja hapa duniani, alibatizwa na alisulubiwa, na akamwaga damu yake ili kutuokoa toka katika dhambi zote za ulimwengu mara moja na kwa wote. Hivyo ni lazima sisi sote tuamini katika Biblia kikamilifu kama ilivyoandikwa. Sisi hatukuweza kukwepa bali kuhukumiwa kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Yesu Kristo alikuja hapa duniani na ametuokoa toka katika dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu. 
Kutoamini katika ukweli huu, ingawa Mungu amezisamehe dhambi zetu zote kama hivi, basi hiyo ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa na Mungu. Mungu amezitoweshea mbali dhambi zote za ulimwengu kasoro dhambi moja iliyobakia ni, “kumdhihaki Roho Mtakatifu” (Marko 3:28-29). Kwa hiyo, wale wanaopenda kwa kweli kupokea ondoleo la dhambi ni lazima wauamini ukweli kuwa Yesu Kristo alibatizwa, akaimwaga damu yake, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametukomboa sisi toka katika dhambi zote za ulimwengu. Mbali na imani hiyo, ni matendo gani mema ambayo yatakuwa ya muhimu sana kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu? Sasa wakati umewadia kwetu sisi ili kuufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho jinsi ulivyo na kisha kuamini katika ukweli huu. 
Kila mtu ni lazima atambue na kuamini kuwa ukweli uliodhihirishwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania uliokuwa umefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ndiyo injili ya wokovu, na kivuli cha Yesu Kristo atakayekuja. Katika suala zima la kuamini katika Yesu Kristo, ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu aliyoimwaga Msalabani ni vitu muhimu sana kwa wokovu wetu na kwa hiyo ni lazima tuviamini vitu hivyo. Ukweli usiokanushwa wala usiobishwa ni kwamba Yesu amewapatia wokovu kwa wale wanaoamini katika ubatizo wake, damu yake aliyoimwaga Msalabani, na ufufuo wake toka kwa wafu, na kwamba mambo haya yote yalifanyika ili kutuokoa sisi toka katika dhambi za ulimwengu.
 

Dhabihu ya Mwana Ambayo Mungu Aliitaka
 
Hebu tugeukie Waebrania 10:5-9: “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketekzwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.”
Je, kifungu hiki kina maanisha nini kinaposema kuwa Mungu hakupendezwa na dhabihu na sadaka? Kifungu hiki kinanukuu toka Zaburi 40:6-7. Kina maanisha kuwa dhambi zote za ulimwengu hazikuweza kutoweshewa mbali vizuri kwa sadaka za kila siku za Agano la Kale, na kwamba ili kutoa sadaka ya dhambi ya kudumu, Yesu Kristo alikuja hapa duniani, alibatizwa, akamwaga damu yake, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu sote. Maana ya Zaburi ya 40:7, inayosema, “Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa)” ina maanisha kuwa Yesu Kristo alikuja hapa duniani na akazioshelea mbali dhambi zote kwa kuwekewa mikono na damu yake aliyoimwaga kama ilivyoandikwa kabisa katika Agano la Kale. 
Katika kipindi cha Agano la Kale, dhambi za watu wa Israeli waliondolewa dhambi zao wakati mnyama wa sadaka ya kuteketezwa alipotolewa kwa Mungu katika Siku ya Upatanisho kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu na kuimwaga damu ya sadaka. Vivyo hivyo, Yesu Kristo aliyekuja hapa duniani ili kufanyika sadaka ya kuteketezwa ya milele kwa wanadamu wote alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kuupokea ubatizo, ambao ni mfano wa kuwekewa mikono, na akabeba adhabu ya dhambi za wanadamu wote kwa kuzipelekea dhambi hizi za ulimwengu Msalabani, alisulubiwa, akaimwaga damu yake ya thamani na kufa. Kwa kufanya hivyo Yesu ametoa wokovu wa milele kwa wote wanaoamini. 
Kwa usahihi kabisa kama Mungu alivyoahidi kwa kupitia utaratibu wa Hema Takatifu la Kukutania, katika Agano Jipya Yesu alikuja hapa duniani na kwa hiyo ameutimiza wokovu mara moja na kwa wote. Kwa hiyo wale wanaoamini wameokolewa toka katika dhambi zote. Katika Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa na ahadi ya Mungu kuwa Yesu atazitoweshea mbali milele dhambi za watu wote mara moja kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake. Na kwa kweli Yesu alikuja na akautimiza wokovu ulioahidiwa kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake na kwa hiyo kulitimiza Neno la Mungu kwa ukamilifu. Kwa maneno mengine, ahadi zote za Mungu za wokovu, kwa kweli zimetimizwa katika Yesu Kristo. 
Watu wa Israeli wanaamini kuwa Sheria ya Agano la Kale na maneno ya manabii ni Neno la Mungu. Lakini wanashindwa kumwamini Yesu Kristo aliyekuja kwetu katika kipindi cha Agano Jipya kuwa ni Mungu au Mwokozi. Watu wote wa ulimwengu huu, wakiwamo watu wa Israeli, ni lazima sasa watambue kuwa Yesu Kristo ni Mungu mwenyewe na wakubali katika mioyo yao kuwa yeye ni Masihi atakayekuja. 
 


Yesu Alikuja Kwa Ajili Gani?

 
Kwa kuwa Yesu alikuja kuyatimiza mapenzi ya Mungu Baba, yeye ni Mwokozi wa wote wanaoamini katika yeye, na alikuja hapa duniani kuzioshelea mbali milele dhambi zao zote. Kama Waebrania 10:10 inavyosema, “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” Ni lazima tutambue vizuri wazi na kuamini kuwa ilikuwa ni kwa mapenzi ya Mungu Baba hata Yesu Kristo akazaliwa hapa duniani, akabatizwa kwa mujibu wa mapenzi ya Baba, na kwamba kwa mapenzi haya alisulubiwa, akamwaga damu yake Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wa wale wanaoamini. Ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu Baba, Yesu Kristo alipaswa kuutimiza wokovu wa mwanadamu kwa kuzitoweshea mbali dhambi zote kwa ubatizo ambao aliupokea na damu aliyoimwaga. Kwa hiyo, Yesu alijitoa kwa hiari kusulubiwa na kwa sababu hiyo akatupatia wokovu mkamilifu. 
Kwa sababu Yesu Kristo alijitoa mwenyewe ili kuzitoweshea mbali sio tu dhambi za watu wa Israeli bali hata dhambi za wanadamu wote, basi sisi tunaweza kuokolewa ikiwa kila mmoja wetu ataamini katika hili katika moyo wake. Katika kipindi cha miaka yake 33 ya uhai, Yesu alibatizwa mara moja tu na kwa hiyo amewaokoa wenye dhambi wa ulimwengu mara moja na kwa wote. Huu ndio wokovu pekee na mkamilifu. 
Kama ambavyo Yesu alivyo zitowesha mbali mara moja dhambi zote zilizofanywa na wanadamu tangu mwanzo hadi mwisho wa ulimwegu, pia ametuwezesha sisi kuokolewa mara moja kwa imani. Kwa kuutoa mwili wake mara moja na kwa wote, Yesu Kristo ametufanya sisi kuwa wakamilifu daima. Kama ambavyo alivyobatizwa na Yohana na kuhumikwa kwa ajili ya dhambi zetu zote kwa kuimwaga damu yake, basi sasa ni lazima tuamini katika injili hii katika mioyo yetu na hivyo kuokolewa toka katika dhambi zetu zote. Kwa mapenzi ya Mungu Baba, Yesu Kristo alikuja hapa duniani ili kuzibeba dhambi zetu zote na kulipa mshahara wa uhai, na alifanikiwa kuufunua wokovu wake wa kweli kwa kupitia upendo wa Mungu kwa mujibu wa mapenzi ya Baba. 
Neno hili kwa kweli ni ukweli ambao wewe na mimi ambao tunaishi sasa katika ulimwengu huu wa sasa tunapaswa kuliamini. Ni lazima tuufunge ubatizo wa Yesu na damu yake aliyoimwaga kwa pamoja na kisha tuamini katika mambo hayo mawili kuwa ni jozi moja ya ukweli inayotuokoa sisi kikamilifu. Ikiwa tutashindwa kufanya hivyo, basi kwa hakika tutapoteza ondoleo la dhambi la milele. Kwa hiyo, ni lazima tuamini kwa mujibu wa Neno la Mungu lililoandikwa, kwa mujibu wa ukweli wa injili ya maji na Roho. Injili ya maji na Roho inatoa mwanga wa wokovu, lakini ikiwa tutaongeza kitu chochote au kupunguza chochote toka katika vitu hivi muhimu toka katika injili tunapoamini katika Mungu, au ikiwa hatuamini katika ukweli kama ulivyo, basi mwanga huu wa injili utapotea, na utafichika na hatimaye kutoweka kabisa. 
Sisi sote hatupaswi kuanguka chini ya upotofu kuwa injili ya maji na Roho ni moja kati ya mafundisho ya kiulimwengu, kana kwamba inafundisha kuwa mtu anaweza kupokea ondoleo la dhambi kwa kupitia maombi yetu ya toba na kwa kumwomba Mungu kutusamehe dhambi zetu za kila siku. Mungu alisema vizuri katika Waebrania 10:11, “Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.” Kwa maneno mengine, alituambia sisi kuwa dhambi ambazo tunazitenda kila siku haziwezi kuoshelewa mbali ati kwa sababu tu tunamwomba Mungu kutusamehe dhambi zetu kila siku kwa imani yetu katika damu na Msalaba. 
Kwa kuwa sadaka ya dhabihu ambayo Yesu Kristo aliitoa kwa Mungu Baba kwa kubatizwa na Yohana na kufa Msalabani ilikuwa ni kamilifu na yenye kufaa kwa wokovu, basi ni kwa kuamini katika sadaka hii ndipo sisi tumeweza kuokolewa. Kwa kuwa dhambi za ulimwengu zilipitishwa kwa Yesu Kristo mara moja na kwa wote wakati alipobatizwa na Yohana ndio maana Yesu aliweza kuzibeba dhambi zetu kwenda nazo Msalabani na kufa juu yake ili kuimaliza adhabu ya dhambi zao, na ni kwa sababu ya tendo hili ndipo dhambi za wote wanaoamini katika ubatizo wake na damu iliyomwagika zimeoshelewa mbali. 
Kwa kuamini katika ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea na damu ya Msalaba, sisi pia tulikufa pamoja na Yesu Kristo na kisha tukafanyika hai pamoja naye kwa imani. Warumi 6:23 inasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Mshahara wa dhambi ni mauti, na kwa hiyo mshahara huu ni lazima ulipwe kwa uhai. Hii ndiyo sababu ilikuwa ni muhimu kwa Yesu Kristo kuja hapa na kufanyika mwili, kubatizwa na Yohana, na kuimwaga damu Msalabani. Kule kuzipitisha dhambi zako kikamilifu katika mwili wa Yesu kulitimizwa kwa ubatizo wake, na kwa kuzibeba dhambi hizi na kufa, Yesu alilipa mshahara wa dhambi zako na kwa hiyo amezitoweshea mbali mara moja na kwa wote. Lakini pamoja na hili, hata pale ambapo Mungu ametupatia sisi ukweli huu wa injili, bado kuna watu wengi ambao bado wanamsihi Mungu kuzisamehe dhambi zao halisi kila siku—kwa kweli hawaufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho. 
Wakati watu wanapokuwa na dhambi katika mioyo yao, hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuogopeshwa mbele za Mungu kwa sababu ya dhambi hizi. Ni kweli kuwa kuna watu wengi ambao bado hawaifahamu injili ya maji na Roho lakini ili waweze kuondolewa dhambi zao wanagubikwa na uoga kwa sababu ya dhambi za dhamiri zao. Hata hivyo, Yesu alikuja hapa duniani kuwakomboa toka katika dhambi zao zote, alibatizwa, akamwaga damu yake Msalabani, na kwa hiyo amewaokoa kikamilifu. Kwa hiyo ni sababu gani itakayotufanya sisi tuogope, wakati injili ya maji na Roho, ambayo ni injili ya wokovu wa Mungu imetuokoa sisi kikamilifu na kulishughulikia suala la adhabu ya dhambi? 
Wale wanaofahamu na kuamini kwa kweli kuwa Yesu amezitoweshea mbali dhambi zote za mwanadamu kwa kupitia injili ya maji na Roho basi wanaweza kwa hakika kuokolewa kikamilifu kwa imani kama Mungu alivyoahidi, “Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; Zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” (Isaya 1:18). Sisi sote tunaweza kuokolewa kwa imani, kwa kuwa kulikuwa na ubatizo wa Yesu ambaye alizipokea dhambi za ulimwengu huu kwa mujibu wa sheria ya Mungu iliyowekwa katika Agano la Kale ambayo ilizipitisha dhambi zote katika sadaka ya kuteketezwa kwa kuwekewa mikono. Ni kwa sababu Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa ndio maana aliweza kufa Msalabani, na kwa kuwa wokovu ambao Mungu aliuzungumza katika Agano la Kale ulitimizwa, basi ndio maana tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa imani yetu tu. 
Lakini pamoja na ukweli huu usioweza kubishiwa, bado tunaona baadhi ya watu ambao wanaamini katika Yesu kana kwamba ni zoezi tu. Wanalia na kuomboleza kila siku ili kuziimarisha imani zao kwa sababu msingi wa imani zao ni kuhuzunika pamoja na Yesu kwa ajili ya mateso ya kifo ambayo aliyapitia pale Msalabani. Mioyo ya watu wa jinsi hiyo kwa kweli imechafuka kabisa na ni lazima waachane na imani hii isiyo sahihi. 
Ni wewe na mimi ambao ndio tunahitaji ubatizo na damu ya Yesu Mwokozi wetu, na wala Yesu hahitaji huzuni zetu na huruma na kujitoa. Ukweli rahisi ni kuwa ni sisi ndio tunaomhitaji Yesu Kristo Mwokozi, lakini bado kuna watu wengi wanaomwamini Mungu pasipo sababu yoyote hali wakifikiri kwamba ni Mungu ndiye anayepungukiwa katika kitu fulani, kana kwamba Mungu anawaomba wao kumwamini yeye. Lakini imani ya jinsi hiyo inayoamini kwa dharau na majivuno ni aina ya imani ambayo inadharauliwa na Mungu. 
Mioyo ya wale ambao wanasema kwa dhihaka kwamba watamwamini yeye, kana kwamba wanamfanyia Yesu upendeleo, inajiweka juu sana kuliko hata Mungu, na kwa hiyo katika ujinga wao hawawezi kukubali katika mioyo yao kuipokea injili ya maji na Roho ambayo inawaokoa wao kikamilifu toka katika dhambi. Hawalizingatii vya kutosha Neno la Mungu kiasi kuwa wanaona ni tofauti na ambavyo majirani zao wanasema, wanaendelea kudhihaki na kulidharau hilo Neno kana kwamba kuliamini Neno ni kama kumfanyia Mungu upendeleo kutokana na huruma zao. 
Hatimaye hao ndio wale wasioamini katika ubatizo na damu ya Yesu iliyomwagika kuwa ni ondoleo lao la dhambi zao na wanasimama kinyume na Mungu. Wanaamini kuwa dhambi zao zinaweza kuoshelewa mbali kwa kupitia maombi yao ya huruma ya toba pasipo hata kuamini katika injili ya maji na Roho. Kwa sababu wanalichukulia jina la Mungu kwa utupu, basi hawafahamu wala hawaamini kuwa Yesu Kristo Mwokozi amezitoweshea mbali dhambi zao, na kwa hiyo hawawezi kuokolewa. 
Mungu alisema, “Nitamrehemu nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye” (Warumi 9:15). Ikiwa Mungu aliamua kuwaokoa wenye dhambi kwa sheria ya wokovu toka katika rehema zake, basi atafanya hivyo kwa hakika kama alivyoamua. Kwa hiyo ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho na hivyo kupokea wokovu wa kweli. 
Wale wasioamini Neno la injili ya maji na Roho watagundua wao binafsi jinsi ambavyo hasira ya Mungu ilivyo kali. Kwa upande mwingine, wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho wataona jinsi ambavyo upendo wa Mungu ulivyo mkuu na ulivyo na rehema. Yeyote atakayezikiri dhambi zake mbele za Mungu na kisha akatambua na kuamini katika injili ya maji na Roho, injili ya Mungu ya wokovu mkamilifu, watakombolewa toka katika dhambi zao zote. 
Wale wanaoamini kuwa Yesu Kristo alizichukua dhambi zao zote katika mwili wake kwa kubatizwa watakombolewa toka katika dhambi zao zote. Na kinyume chake, wale wanaoudharau ukweli huu watakabiliana na adhabu ya dhambi ya kutisha kwa ajili ya dhambi zao. Hivyo watu wote wa ulimwengu huu ni lazima waamini katika injili ya maji na Roho ambayo ni ukweli halisi. Wenye dhambi ambao hawaiogopi hukumu ya Mungu na hawaamini katika injili ya maji na Roho basi kwa hakika watahukumiwa kwa dhambi zao. Lakini wale wanaoamini katika ukweli wa Yesu kuziosha dhambi wataokolewa toka katika dhambi zao zote. 
Kila watu ambao dhamiri zao zina dhambi ndani yake wanajaribu kuzifariji dhamiri zao wenye mashaka na mfadhaiko kwa kuja na mafundisho ya wokovu yasiyo na msingi ambayo ni tofauti kabisa na injili ya maji na Roho. Kuna hata wale wanaosema, “kwa kuwa ninaamini katika Yesu, basi ni sawa kwangu kuwa na dhambi katika moyo wangu.” Lakini ni lazima tusisahau kuwa wale wote walio na dhambi katika mioyo yao watakutana na adhabu ya kuzimu, kwa kuwa Mungu ataitoa adhabu yake ya haki kwa watu wa jinsi hiyo kwa ajili ya dhambi zao. Kwa kuwa wapo upande wa Shetani Mungu hawezi kuwaacha peke yao. 
Lakini wale wanaofahamu kuhusu haki ya Mungu, ya kwamba kutakuwa na hukumu yake ya dhambi basi wanamwomba Mungu kwa ajili ya upendo wake wenye rehema hali wakitaka kuokolewa toka katika dhambi zote, wakiutafuta ukweli, na hali wakitamani kusimama upande wa Mungu. Kwa watu wa jinsi hiyo, hapa kuna ukweli kwamba Yesu Kristo alizichukua katika mwili wake dhambi zote za mwanadamu kwa kubatizwa. Kila mwenye dhambi ni lazima aamini katika ukweli huo na kisha apokee ondoleo la dhambi. Kwa kupitia ubatizo wake, Yesu Kristo alizipokea dhambi zote za ulimwengu mzima mara moja na kwa wote, akafa Msalabani mara moja, na kwa hiyo amezitoweshea mbali dhambi zote na kutufanya sisi kuwa wenye haki. 
Kwa kupitia injili ya maji na Roho, sisi sote ni lazima tutambue kuwa wokovu wetu wa kweli ni upi, na ni lazima tuwe na imani katika mioyo yetu inayoamini kwa kweli katika injili hii. Wote wanaoamini katika ukweli huu katika mioyo yao, bila kujalisha dhambi ambazo watakuwa wamezifanya, basi kwa hakika wataoshwa toka katika dhambi zao zote kwa imani na kisha watapokea ondoleo la kweli la dhambi na kupata uzima wa milele. Je, hupendi kuamini katika Neno hili la injili na kuipokea injili ya maji na Roho kwa imani, injili ambayo inazifanya dhambi zote za moyo wako kutoweka? Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho kwa hakika watapokea ondoleo la dhambi mbele za Mungu.
 


Sala Zako za Toba Haziwezi Kukuokoa

 
Siku hizi, wale wanaosema kuwa wanamwamini Yesu wanatoa sala zao za toba kila siku hali wakimwomba Mungu kuzisamehe dhambi zao. Wanaishi maisha yao ya imani kwa kutoa sadaka zao za kuteketezwa kwa Mungu kila siku kama ilivyokuwa katika kipindi cha Agano la Kale. Lakini haya si maisha ya imani ambayo utapenda kuyaishi. Je, Yesu aliimwaga damu yake Msalabani ili kuziosha dhambi zako kila unapotoa sala zako za toba? Kwa kweli sio hivyo. Badala yake, ni lazima uzioshelee mbali dhambi zako mara moja na kwa wote kwa kuamini kuwa nguvu ya ubatizo na damu iliyomwagika ya Yesu Kristo inadumu milele. Wale wanaojaribu kuoshwa dhambi zao kwa kutoa sala za toba kila siku hawawezi kupokea ondoleo la dhambi la milele na wala hawana imani inayowawezesha wao kupokea wokovu wa kweli. 
Ikiwa dhambi za mtu yeyote zingeliweza kusamehewa kwa kupitia sala za jinsi hiyo za toba au taratibu zozote za kidini zilizoundwa na mwanadamu, basi Mungu asingekuwa ameanzisha sheria ambayo inatangaza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Ili watu waweze kuondolewa dhambi zao, basi ni lazima watoe sadaka inayozipitisha dhambi zao katika mwili wa Yesu kwa imani. Tunachotakiwa kuwa nacho si aina ya imani inayotoa maombi ya toba kila siku, bali imani inayoamini katika injili ya maji na damu iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. Kwa maneno mengine, ni lazima tutambue kuwa ni imani tu inayoamini katika injili ya maji na Roho ndiyo inayoweza kutuletea sisi uoshwaji wa kweli wa dhambi, na ni lazima tuuamini ukweli huu katika mioyo yetu. 
Kama ambavyo wenye dhambi wa Agano la Kale walivyozipitisha dhambi zao juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yao juu ya kichwa chake wakati walipotoa sadaka yao ya dhambi, basi sisi nasi ni lazima tuzipitishe dhambi zetu juu ya Yesu Kristo kwa kuamini katika ubatizo wake, na kwa imani hii inayoamini katika ubatizo wake na damu yake iliyomwagika Msalabani basi tunaweza kwenda kwa Mungu na kupokea ondoleo la dhambi la milele. Mungu alisema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu,” na “Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:10, 17).
Yoahana 1:29 inasema, “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Kifungu hiki kinaelezea ushuhuda ambao Yohana Mbatizaji aliutoa siku ya pili yake baada ya kuwa amembatiza Yesu. Wakati Yohana Mbatizaji alipomwona Yesu anamkaribia alisema, “Tazameni nyie watu! Hapa yupo yule mmoja!” Jambo hili lilisababisha msukumano katika lile kundi lililokuwa limekusanyika kumzunguka Yohana. Yohana akapiga kelele akasema, “Tazama! Anakuja hapa Mwanakondoo wa Mungu! Si mwingine bali ni Mwana wa Mungu, Mwanakondoo halisi wa Mungu ambaye alizichukua dhambi za wanadamu katika mwili wake kwa kupitia mimi. Yeye ni Mwokozi wetu. Yeye ni Yesu Kristo, Mwanakondoo wa Mungu. Tazama! Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” 
Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa amembatiza Yesu Kristo na akawa amezipitisha dhambi za ulimwengu katika mwili wake, basi ndio maana Yohana mwenyewe aliweza kumshuhudia Yesu. Kwa maneno mengine, kwa kuwa Yohana alikuwa amezipitisha dhambi zetu juu ya Yesu kwa kumbatiza, ndio maana Yesu alifanyika kuwa Mwanakondoo wa dhabihu ya kuteketezwa ambaye alizichukua dhambi zetu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu Baba. 
Katika Agano la Kale, ondoleo la dhambi lilipokelewa kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu, lakini katika Agano Jipya, tunaweza kuondolewa dhambi zetu kwa imani inayoamini kikamilifu katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Kwa kuwa Mungu alipokea wanyama kama mafahari ya ng’ombe, mwanakondoo, na mbuzi kuwa ni sadaka ya kuteketezwa ili kuziondolea mbali dhambi za watu wa Israeli, wanyama wengi waliuawa, na kukatwa katika vipande, na kuchomwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Mamilioni ya wanyama wa kuteketezwa kwa kweli waliuawa kwa sababu ya dhambi za watu. 
Lakini katika kipindi cha Agano Jipya, Yesu hakutoa sadaka za wanyama kama hao wa kuteketezwa, lakini aliutoa mwili wake mwenyewe kwa ajili yetu. Kwa kuwa Yesu Mwanakondoo wa Mungu alikuja hapa duniani, akazipokea dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake na akamwaga damu yake Msalabani, basi amewawezesha wale wanaoamini katika hili kuokolewa toka katika dhambi zao zote mara moja na kwa wote. Yesu alikuja kwetu ili kuzimaliza kabisa dhambi zetu milele kwa maji, damu, na Roho. 
 Sasa Mungu anakuamuru wewe na mimi kuamini katika ukweli huu wa wokovu halisi. Mungu anatueleza sisi kuwa, “nimezitoweshea mbali dhambi zako zote, kwa kuwa nilikuwa nawapenda. Nimewaokoa ninyi kama hivi. Kwa hiyo uamini! Nimezitoweshea mbali dhambi zako kwa kuwapatieni Mwana wake mwenyewe kama sadaka ya dhambi kwa ajili yenu. Nilimruhusu Mwana wangu kuishi hapa duniani kwa miaka 33 ya uhai, nilimfanya abatizwe, nilimfanya aimwage damu yake Msalabani kwa ajili yako, na kwa kufanya hivyo nimekukomboa wewe kikamilifu toka katika dhambi zako zote na adhabu ya dhambi. Sasa, kwa kuamini katika ukweli huu mnaweza kufanyika watoto wangu ninaowapenda, ninaoweza kuwakumbatia katika mikono yangu.” Fahamu na uamini hivi katika moyo wako—wale wanaoamini katika ubatizo wa Yesu Kristo alioupokea na damu yake aliyoimwaga wataokolewa toka katika dhambi zao zote na pia watapokea haki ya kuwa wana wa Mungu mwenyewe. 
 
 

Je, Ni kweli Kuwa Yesu Aliziondoa Dhambi Zote za Ulimwengu Huu?

 
Hebu tugeukie Waebrania 10:14-18: “Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye ameshuhudia; kwa maana, baada ya kusema, Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika nia zao nitaziandika. Ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”
Kifungu kinaweka wazi: “Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.” Hebu sikiliza habari hizi zilizobarikiwa, kwamba dhambi zetu zote zilipitishwa kwa Yesu kwa kupitia ubatizo alioupokea! Sio tu kwamba dhambi zangu na zako tu ndizo zilipelekwa kwa Yesu, bali dhambi zote za wanadamu wote zilipitishwa kwa Yesu kikamilifu. Ili kuitimiza haki yote ya Mungu, Yesu alipokea kule kuwekewa mikono, alibatizwa ndani na nje ya maji na hivyo akaziruhusu dhambi zote kuhamishiwa kwake mwenyewe. 
Zaidi ya yote, hali akiwa amezibeba dhambi zote alisulubiwa, na hivyo akabeba adhabu ya dhambi zote za mwanadamu, na kwa hiyo wale wote wanaoamini wamekombolewa toka katika hukumu zao zote. Kama ambavyo Kuhani Mkuu alivyozipitisha dhambi za watu wa Israeli kwa mnyama wa sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa chake, Yohana Mbatizaji alizipitisha dhambi zetu zote kwa Yesu kwa kumbatiza. Na Yesu kwa upande wake, alizibeba dhambi hizi na alisulubiwa na hivyo amemkomboa kila mtu anayemwamini yeye toka katika dhambi. Kwa hiyo, wale wanaoamini katika hili wanaweza kupokea haki ya kufanyika watoto wa Mungu mwenyewe. 
Warumi 10:10 inasema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Kwa watu wote, ni kwa kuamini katika haki ya Mungu kwa moyo ndipo wanapoweza kuhesabiwa haki, kwa kuamini katika ukweli wa wokovu kwa moyo ndipo wanapoweza kupokea ondoleo la dhambi na kuingia Mbinguni. Akina kaka na akina dada, je, mmeokoewa kwa kuamini kwa mioyo yenu na kukiri kwa ndimi zenu kuwa ubatizo na damu ya Yesu ni vitu muhimu vinavyoiunda “haki ya Mungu”, “ukweli wa wokovu,” na “injili ya ondoleo la dhambi”? Chini ya utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa wa Agano la Kale, dhambi za waisraeli hazikuondolewa kwa sababu tu ya kule kumchinja mnyama wa sadaka ya kuteketezwa pasipo kuwekea mikono ambako ndiko kuliko zipitisha dhambi zao kwenda katika mnyama wa sadaka ya kuteketezwa. Vivyo hivyo, ikiwa tunaamini katika damu ya Msalaba tu na kisha kuuacha ubatizo ambao Yesu aliupokea, basi dhambi zetu zote haziwezi kuoshelewa mbali. 
“Ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la haya likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:17-18). Kwa nini Mungu anasema hapa kuwa hatazikumbuka tena dhambi zetu? Pamoja na kuwa hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi hadi siku ile tutakapokufa, na kwa kuwa Yesu alikwisha zichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kubatizwa, wokovu wetu kwa sasa umekamilika na utadumu milele, na sisi ambao tunaamini katika ukweli huu kwa sasa hatuna dhambi. Hii ndiyo sababu Mungu hana sababu ya kuzikumbuka dhambi zetu. 
Haki ya Mungu ina maanisha uhalali wa kazi zake. Haki ya Mungu Baba inatueleza sisi kuwa kama Mungu alivyo mtakatifu, wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho pia ni wakatifu na wasio na dhambi. Tangu mwanzo, Mungu alitupenda sisi na alitamani sana kutufanya sisi kuwa watoto wake mwenyewe. Lakini kila alipotaka kutufanya sisi kuwa watoto wake alishindwa kwa sababu ya dhambi zetu. Kwa hiyo Mungu Baba alikuja na suluhisho ili kutatua tatizo hili. 
Kwa sababu Mungu alikuwa ameweka pembeni sadaka isiyo na mawaa ambayo itasulubiwa kwa haki kwa niaba yetu na akaamua kuzioshelea mbali dhambi zetu kwa kuzipitisha dhambi zote juu ya sadaka hii ya kuteketezwa, basi Yesu hakusita kubatizwa ili kufanyika sadaka yetu ya dhabihu, kuhukumiwa kwa haki kwa niaba yetu, na kwa hiyo kutoa sadaka ya dhambi ya kudumu. Na kwa kupitia sadaka hii ya dhambi, Mungu aliyatimiza majaliwa yake ya kuwasafisha wote wanaoamini kuwa wameokolewa toka katika dhambi zao na kisha kuwafanya kuwa watoto wake mwenyewe. Sasa, wale wanaoamini katika injili hii ya kweli wameondolewa toka katika dhambi zao zote mbele za Mungu. Kwa kuwa Yesu amekwisha zioshelea mbali dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa, ikiwa tutaamini katika huyu Yesu ambaye amezisafishilia mbali dhambi za mwanadamu kwa kuhukumiwa kwa haki, kwa hiyo hatuhitajiki tena kutoa sadaka yoyote kwa ajili ya dhambi zetu. Kaka zangu na akina dada, Je, bado tunahitaji kutoa dhabihu kwa sababu ya dhambi zetu? Hapana, kwa kweli si hivyo!
Je, unafahamu ni kwa nini Yesu Kristo alisulubiwa pamoja na kuwa alikuwa hana dhambi na msafi? Ingawa Yesu alisulubiwa, yeye alikuwa hajafanya kosa lolote linalomfanya astahili kufa. Ila ni kwa sababu alikuwa amezipokea dhambi zote za mwanadamu kwa kubatizwa katika Mto Yordani na ndio maana alipaswa kufa kwa niaba yetu. Sababu iliyomfanya Yesu kufa Msalabani ni kwa sababu alikuwa amekwisha zipokea dhambi za ulimwengu zilizokuwa zimepitishwa kwake kwa kupitia ubatizo wake na alikuwa tayari kuitimiza haki yote. 
Wakati Mwana wa Mungu alipobatizwa ili kuitimiza haki yote kwa njia hii, kwa nini basi tusimshukuru? Kwa sababu Yesu alikuwa amezichukua dhambi zetu katika mwili wake ndio maana Yeye, kama kondoo mbele yao wamkatao manyoya yake, alibeba kwa kimya mateso ya Msalaba. Ni lazima sisi sote tuukumbuke ubatizo wake na Msalaba daima, ikiwa kama Yesu asingalisulubiwa na kuhukumiwa adhabu kwa ajili yetu, basi ingalitupasa sisi wenyewe kuhukumiwa kwa hakika. 
Bwana wetu sio tu kwamba alizichukua katika mwili wake dhambi zetu zote, bali yeye mweneywe alibeba pia adhabu ya dhambi. Kwa lugha nyingine, Yesu ni Mwokozi yeye mwenyewe, ambaye amezichukua dhambi zetu zote katika mwili wake, alifanyika kuwa sadaka ya dhambi zetu binafsi na alibeba kimyakimya adhabu ya dhambi Msalabani, alifanya yote haya ili aweze kutuokoa toka katika dhambi na hivyo kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la haya likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. Basi ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu” (Waebrania 10:17-19).
Je, unafahamu sasa kuwa ni kwa nini Yesu Kristo alisulubiwa? Hatupaswi kuamini katika damu ya Yesu ya Msalaba tu, bali tunapswa kufahamu kuwa ni kwa nini ilimpasa kufa Msalabani, na pia ni lazima tufahamu kikamilifu na kuamini kuwa kwa sababu hii imani inasimama katika ubatizo ambao aliupokea. Ikiwa wewe na mimi tunapenda kufahamu na kuamini kikamilifu kuhusu ni wapi na kivipi dhambi zetu zilioshelewa mbali basi ni lazima tutambue na kuamini kwamba ni kwa sababu dhambi zetu zilikuwa zimepitishwa kwa Yesu wakati alipobatizwa na Yohana katika Mto Yordani na ndio maana tumeoshwa toka katika dhambi zetu kwa imani. 
 


Sasa Tunaweza Kuokolewa Toka Katika Dhambi Zetu Zote Kwa Kufahamu na Kuamini katika Ukweli wa Injili ya Maji na Roho

 
Nilichokuambia hadi sasa ni ukweli wa injili ya maji na Roho ambao Biblia inauzungumzia kwa kina. Na ukweli huu ni wokovu ambao ulikuwa umepangwa hata kabla ya misingi ya ulimwengu, na wokovu huu pia unadhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambavyo ni vifaa vilivyotumika katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. Mimi pamoja na wafanyakazi wenzangu, nimekuwa nikiuhubiri ukweli huu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kwa watu wengi sana ulimwenguni. Na hata sasa, katika saa hii, injili hii inaendela kuenea katika ulimwengu mzima kwa kupitia vitabu vyetu. 
Hata hivyo, bado kuna wale wanaodai kumwamini Yesu hata pale ambapo hawaifahamu injili ya maji na Roho. Ninaweza kudiriki kuwaita watu wa jinsi hiyo kuwa ni wapumbavu, kwa kuwa injili hii ya maji na Roho ndio kiini cha ukweli unaotueleza sisi vizuri juu ya utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa uliotimizwa kwa kupitia Yesu Kristo, ambaye ni kiini cha kweli cha kivuli cha wokovu kilichodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Sasa ni wakati wako. Ikiwa ulikuwa unaamini pasipo kuufahamu ukweli halisi, basi sasa ni wakati wako kwa wewe kugeuka, kuamini katika injili ya maji na Roho na kisha kupokea ondoleo la dhambi zako. 
Ubatizo wa Yesu na kifo chake juu ya Msalaba vilikuwa vimeahidiwa hata kabla ya misingi ya ulimwengu, na vilikuwa vimedhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ili kuitimiza ahadi hii, na ili kukuokoa wewe na mimi kikamilifu toka katika dhambi zetu, Yesu alibatizwa, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na sasa ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu Baba. 
Je, bado unajaribu kumfuata Yesu kwa kufuata uzoefu wako binafsi na mihemko yako pasipo kuutambua ukweli huu? Kuna watu wengi wa jinsi hiyo katika ulimwengu huu, lakini sasa ni lazima wageuke toka katika imani yao potofu na kisha waamini kwa mioyo yao yote katika ukweli wa injili ya maji na Roho uliojificha katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizodhihirishwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. 
Waebrania 10:19-20 inasema, “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake.” Wakati Yesu Kristo alipokuwa amekwisha kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, na kusulubiwa, pazia la Hekalu lilipasuka, na dhambi za mwanadamu zilioshelewa mbali kwa ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Pazia la Hekalu lililokuwa limefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa lilikuwa gumu sana kiasi kuwa halikuweza kupasuka hata pale lilipovutwa katika kona zake nne na farasi wanne. 
Hilo ndio lile pazia gumu la Hekalu ambalo lilipasuliwa toka juu hadi chini, pamoja na kuwa pazia hilo lilikuwa halijaguswa na mtu yeyote, kupasuka kwa pazia hilo kunaonyesha wazi kuwa wakati ule Yesu alipoukamilisha utume wake, malango ya Mbinguni yalifunguliwa. Kule kupasuka kwa pazia la Hekalu toka juu hadi chini kuna maanisha kuwa kuta zote za dhambi zilivunjwa, Mungu alituonyesha sisi kwa kupitia Yesu Kristo kuwa amezivunja kuta zote za dhambi. 
Ni nini basi kinachomaanisha kuwa kuta za dhambi ziliangushwa chini? Hii inamaanisha kuwa mtu yeyote anaweza kuondolewa dhambi zote kwa kuamini katika ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea na damu yake Msalabani. Kitu ambacho Mungu alifikiria kukidhihirisha kwa kupitia mlango wa Hema Takatifu la Kukutania ni kwamba wokovu wa mwanadamu sasa umetimizwa mara moja na kwa wote kwa kupitia huduma za Yesu zinazoonyeshwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa sababu upatanisho wetu wa kudumu uliokuwa umeahidiwa na Mungu kwetu sote ulitimizwa ndio maana pazia la Patakatifu pa Patakatifu lililokuwa limefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa lilipasuka katika vipande viwili toka juu hadi chini, si kwa mkono ya mwanadamu bali kwa mkono wa Mungu mwenyewe. 
Hii inaonyesha kuwa Yesu Kristo aliyefanyika kuwa dhabihu ya kudumu kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ametuokoa sisi kikamilifu tunaoamini katika injili ya maji na Roho. Mungu Baba amepanga kuwa yeyote anayeamini katika ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani anaweza kupokea ondoleo la dhambi na kusimama mbele ya uwepo wake. Je, utaamini katika ukweli huu au la? 
Kama ambavyo Mungu amekupenda wewe, ndivyo Yesu Kristo Mwana wa Mungu alivyokupenda wewe na amekupatia wokovu mkamilifu kwa kubatizwa na Yohana na kusulubiwa. Kwa kupokea upendo huu wa Mungu ambao Mungu ametupatia kwa kupitia Yesu Kristo, na kwa kuamini katika ukweli unaotuwezesha sisi kuingia katika Ufalme wa Mungu, basi dhambi zetu zote zimetoweka. Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho basi hata dhambi zetu halisi zimeshughulikiwa, kwa kuwa dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi zilikwisha oshelewa mbali kwa ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. 
Waebrania 10:22 inasema, “Na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.” Biblia inaendelea kuongea juu ya kuosha dhambi. Sisi tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuamini katika ukweli kuwa Yesu Kristo ameziosha mbali dhambi zote tunazozifanya kwa miili na mawazo yetu kwa kupitia ubatizo wake. 
Kama ambavyo Kuhani Mkuu alivyo uoshea mbali uchafu wake katika birika la kunawia baada ya kutoa sadaka, baada ya kuzisafisha dhambi zetu zote kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu, sisi pia, ni lazima tuikumbuke imani hii kila siku. Kama ambavyo Kuhani Mkuu alivyojiosha mwenyewe katika birika la kunawia la shaba, sisi ni lazima tuzioshelee mbali dhambi zetu halisi kwa kukumbuka na kuamini kila siku kuwa dhambi zetu zote zilisafishiwa mbali kwa ubatizo wa Yesu, kwa kuwa kadri tunavyoishi hapa ulimwenguni kuna nyakati ambapo tunakuwa katika hali ya kukumbwa na ule uchafu wake. 
Dhambi zote, kwamba zimefanyika kwa mwili, moyo, au mawazo zinatokana na dhambi za ulimwengu. Ni imani ipi inayoweza kutusaidia kuzisafisha dhambi hizi, je, tunaweza kuzioshelea mbali hizo dhambi zote za ulimwengu? Tunaweza kuzioshelea mbali kwa ubatizo ambao Yesu aliupokea. Wale ambao mara moja walifanyika kuwa safi kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu ni lazima waitunze mioyo yao kuwa safi, na kila wanapotenda dhambi ni lazima waioshe tena kwa imani. Wale wanaoukumbuka ubatizo wa Yesu kila siku na kuyaosha mavazi ya matendo yao kwa imani hao ndio waliobarikiwa. Kwa kuwa dhambi zetu zote zilipitishwa kwa Yesu Kristo kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana, basi kwa kuutafakari ukweli huu na kisha kuuamini kila siku tunaweza kukombolewa kikamilifu toka katika dhambi zetu milele. 
Ni lazima uamini katika injili ya maji na Roho, kuwa dhambi zako zilipitishwa kwa Yesu Kristo wakati alipabatizwa na Yohana. Huna kitu cha kukipoteza kwa kuamini katika injili hii kwa kuwa Mungu mwenye nguvu alikwisha ipanga hata kabla ya misingi ya ulimwengu, kabla ya zama za Agano la Kale. Ule ukweli kuwa Yesu alizipokea dhambi zako kwa kubatizwa katika Mto Yordani na akabeba adhabu ya dhambi zako kwa kwenda Msalabani basi amekuwezesha wewe kuifikia haki ya Mungu na wokovu wako. Ukweli uliokuwezesha kutambua kuwa Yesu Mfalme wa wafalme amekuokoa wewe milele toka katika dhambi, na kwamba ameunyunyizia moyo wako toka katika dhamiri mbaya na ameiosha miili yenu kwa maji safi, basi ukweli huo ni injili hii ya maji na Roho. Injili ya maji na Roho ni Neno la Mungu la msingi kwa maisha yako na linang’aa zaidi wakati unapoamini. 
Wakati wa miaka 3 ya huduma yake ya wazi, kitu cha kwanza ambacho Yesu alikifanya ili kuwaokoa wanadamu wote toka katika dhambi ilikuwa ni kubatizwa. Kwa maneno mengine, Yesu Kristo alipaswa kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake, na ili kufanya hivyo alipaswa kwenda kwa Yohana ili abatizwe naye. Kwa hiyo, injili zote nne zinaandika tukio hili muhimu pale mwanzoni. 
Kwa kweli wewe na mimi tulifungwa ili kuuawa kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini nini kilitokea? Bwana wetu alikuja hapa duniani akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, akafanyika kuwa Mwanakondoo wa Mungu, akazibeba dhambi zote za ulimwengu hadi Msalabani, alipigiliwa misumari katika mikono yake miwili na miguu kwa ajili ya dhambi zetu, aliimwaga damu yote iliyokuwa katika moyo wake na akafa, na kisha akafufuka tena toka kwa wafu. Hii ndiyo sababu Yesu alisema, “Imekwisha,” alipokuwa akivuta pumzi yake ya mwisho pale Msalabani. 
Kila kitu ambacho Yesu alikifanya na kukitenda ni kweli. Yesu alifanyika sadaka yetu ya dhambi ili kutuokoa sisi, na akafufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu. Na baada ya kufufuka toka kwa wafu, alibeba ushuhuda kwa ufufuko wake kwa siku 40, akapaa mbinguni na sasa ameketi katika mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Baba. Huyu Yesu Kristo atakuja hapa duniani ili kutuchukua. Yesu alikuja kama Mwokozi wakati alipokuja kwa mara ya kwanza hapa duniani, lakini atakapokuja tena mara ya pili, atakuja kama hakimu kuwahukumu wote ambao hawakuamini. 
Ni lazima sasa utambue kuwa Yesu Kristo atarudi hapa duniani kama hakimu, na kuita na kuwapokea kama watoto wa Mungu wale walioamini katika wokovu wa maji, damu, na Roho alivyovitimiza katika miaka 33 ya uhai wake hapa duniani na kisha atawawezesha kuishi katika utawala wa Milenia na Mbingu ya milele, na kisha kuitoa hukumu yake ya milele kwa wale ambao hawaimini injili ya maji, damu, na Roho na walioukataa upendo wa Mungu. 
Sasa, hupaswi tena kuidharau injili ya maji na Roho na kujifanya kuwa huifahamu, bali ni lazima uamini katika ukweli huu wa wokovu. Ni lazima utambue kuwa kama ambavyo Mungu aliahidi kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania na utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa, Yesu Kristo alikuja hapa duniani, alibatizwa katika muundo wa kule kuwekewa mikono, alisulubiwa na kwa hiyo ameyaokoa mataifa yote ya ulimwengu mzima toka katika dhambi zao zote, na ni lazima upokee ondoleo la dhambi zako kwa kuamini katika ukweli huu kwa moyo wako wote. 
Hata hivyo, taifa la Israeli bado limegeuza mgongo toka katika ukweli na linamsubiri Masihi mwingine. Lakini waisraeli ni lazima watambue kuwa bila kujalisha jinsi wanavyosubiri kwa hamu kuja kwa Masihi mwingine zaidi ya Yesu, kwa kifupi tu ni kuwa hakuna Masihi mwingine zaidi ya Yesu Kristo. Kule kusema kuwa hakuna Masihi mwingine bali ni Yesu katika uso wa dunia hii huo ni ushahidi mwingine binafsi wa kweli, na kwa kuwa waisraeli hawabaguliwi kuhusu ukweli huu, basi hata kwao hakuna Masihi mwingine zaidi ya Yesu Kristo. 
Kwa hiyo, watu wa Israeli ni lazima watubu toka katika dhambi zao za kutokuamini katika Yesu Kristo kuwa ni Mwana wa Mungu, na ni lazima waamini kuwa Yesu Kristo ndiye Masihi wa kweli kwa hakika na kisha waipokee imani hii kuwa ni ukweli. Kwa mara nyingine kwa kuthibitisha na kuamini kuwa Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa kweli atakayekuja, basi taifa la Israeli litafanyika kuwa taifa la kweli la kiroho lililochaguliwa na Mungu. 
Hata sasa, watu wa Israeli bado wanasubiri kuja kwa Masihi wa kushangaza, mwenye uwezo, na mwenye nguvu ambaye atawaokoa toka katika mateso na mahangaiko ya ulimwengu. Lakini Yesu Kristo alikwisha kuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu kama Masihi na aliwaokoa wanadamu ambao wasingeweza kukwepa hukumu ya moto toka katika dhambi zao zote. Kwa hiyo, ni lazima waukubali ukweli huu na kisha wauamini. Yesu mwenyewe alikuja hapa duniani kama sadaka ya dhambi iliyokuwa imeahidiwa katika Agano la Kale kwa ajili ya nafsi zao, amewaokoa wao milele toka katika dhambi zao na amewafanya wao kuwa watu wa Mungu mwenyewe. 
Yesu Kristo ambaye alikuja kama Mwokozi ametuokoa sisi sote kwa kupitia injili ya maji na Roho, ambao ni ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Na kweli atatuwezesha sisi tunaoamini katika ukweli huu kutawala pamoja naye katika Ufalme wa Milenia pamoja naye. Baada ya hili, atawaruhusu pia kushiriki katika Ufalme wa milele wa Mungu na kuishi milele pamoja na Mungu mwenyewe katika furaha na utukufu. 
Kwa hiyo, wakati bado tupo hapa duniani, sisi sote ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho kwa mioyo yetu na kufanyika watoto wa Mungu. Ni wale tu wanaoamini katika injili hii ya kweli ndio wanaoweza kufanyika wana wa Mungu wasio na dhambi na walio na uhakika wa kupokea baraka zote ambazo zinawasubiri katika ulimwengu unaokuja. 
Halleluya! Ninamshukuru Bwana kwa imani yangu kwa kutupatia baraka za kiroho za Mbinguni. Bwana wetu aliahidi kuwa atakuja mara; hata sasa, na uje Bwana!