Search

ခရစ်ယာန်ယုံကြည်မှုနှင့်ပတ်သက်သောမေးခွန်းများ

ဘာသာ ၂ - သန့်ရှင်းသောဝိညာဥ်တော်

2-2. Je Roho Mtakatifu huweka makazi ndani endapo utaendelea kuamini Injili ya maji na Roho au je kwa wakati mwingine huwa nje pembeni na kuja ndani yako pale unapo omba msaada?

Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwa maneno mengine. Mungu alitupatia sisi sote tulio wa haki kwake neema ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na Roho tokea pale Yesu alipo batizwa na Yohana mbatizaji, akafa msalabani na kufufuka (Yohana 15:26). Waefeso 1:13 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema ya wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye wa kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.” Roho Mtakatifu huja kwa wale wenye haki ambao wamekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kumwamini Yesu Kristo na hivyo moja kwa moja kutiwa muhuri kama watoto wa Mungu.
Katika Yohana 14:16 Bwana alisema “Nami nitamwomba Bwana naye atawapa Msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele”. Wafuasi wa Yesu walipokea msamaha wa dhambi zao zote kwa kuamini kwamba Yesu alizibeba dhambi hizo zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake, na hii ndiyo kupelekea kwa Yohana Mbatizaji kusema. “Tazama Mwanakondoo wa Mungu alichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29).
“Dhambi ya ulimwengu” ni dhambi zote za watu wote ulimwenguni walizo tenda tokea mwanzo hadi mwisho wa dunia. Alikubali kuzibeba dhambi za ulimwengu mara moja, kufa msalabani, alifufuka na kwa jinsi hiyo alitufanya kuwa wenye haki daima. Katika Waebrania 10:12-14 imeandikwa “Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo majo amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.”
Bwana alibatizwa na Yohana, alisulubiwa ndipo alifufuka na hivyo kutufanya wenya haki daima. Tulisamehewa dhambi zetu zote mara moja na kuwa watoto wa Mungu kupitia Yesu na ukweli huu hauwezi kufutika hata milele. Wale walio wenye haki kupitia imani hii hawana dhambi moyoni mwao. Ingawa watu hawatoweza kujizuia kutenda dhambi kutokana na udhaifu, lakini bado hawana dhambi daima kwa sababu Yesu alikwisha zibeba dhambi zote. Hivyo kamwe hawataweza kuwa wenye dhambi.
Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya mioyo ya wenye haki walio takaswa daima. Hatutoweza kujizuia kutenda dhambi kutokana na udhaifu lakini ikiwa tunajikuta tunatenda dhambi mara kwa mara basi karama ya Yesu Kristo aliyetufanya kuwa wenye haki daima itakuwa ni bure, na itamlazimu afe kwa mara nyingine tena baada ya kubeba dhambi hizo. Hii ndiyo dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu (Waebrania 6:4-8, 10:26-29).
Hivi ndivyo Roho Mtakatifu awekavyo makazi ndani ya wale walio na haki ambao wanapokea msamaha wa dhambi na kuzaliwa upya kwa kuamini Injili ya maji na Roho Paulo alisema, “Kwa kuwa wewe ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alisema: Nitaakaa ndani yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (2 Wakorintho 6:16).
Roho Mtakatifu wakati wote huweka makazi ndani ya watoto wa Mungu wale walio takaswa dhambi zao daima, neno “Kuweka makazi” hapa halina maana kwamba huwa nje kwa kuzunguka huku na kule na kuja ndani yetu pale tunapo fanya maombi na kumwita, bali “hukaa ndani yetu daima” Hukaa ndani ya wale wote walio kwisha zaliwa upya kwa maji na Roho akiwafundisha mambo yote na kuwaongoza katika kulielewa neno la Mungu (Yohana 14:26).
Hivyo, yeyote asiye na Roho Mtakatifu si wa Mungu (Warumi 8:9). Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya wale wote walio takaswa dhambi zao akiwafundisha mambo yote ya mbinguni na kuwashuhudia ya kwamba wao ni watoto wa Mungu. Si kweli kwamba Roho Mtakatifu hukaa karibu nasi akija kwetu kama thamani ya juhudi zetu binafsi; badala yake hukaa ndani ya watoto wa Mungu walio zaliwa upya kwa maji na kwa Roho.
Hata hivyo watu wengi hawana ufahamu huu na hivyo kujaribu kumpokea Roho huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao. Na matokeo yake hudhani ya kwamba huja juu yao pale wanapofanya juhudi binafsi katika maombi ya kutubu na huwaacha pale wanapo tenda dhambi. Na hii ndiyo imani ya wale wote ambao bado hawajapokea msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu. Wale wote walio na imani ya kweli huamini ya kwamba wataweza kumpokea Roho Mtakatifu na kuweka makazi ndani yao ikiwa ni ishara ya zawadi baada ya kusamehewa dhambi zao. Imewapasa watu kuachana na mawazo binafsi na kuirudia imani katika neno la Mungu.