Search

ခရစ်ယာန်ယုံကြည်မှုနှင့်ပတ်သက်သောမေးခွန်းများ

ဘာသာ ၃ - ဗျာဒိတ်ကျမ်း

3-1. Je, namba 144,000 katika sura ya 7 ina maanisha kiuhalisia juu ya watu wa Israeli ambao wataokolewa, au ni namba katika lugha ya picha?

Namba 144,000 inayoonekana katika sura ya 7 inatueleza kiuhalisia kwamba ni Waisraeli wangapi ambao wataokolewa katika nyakati za mwisho, watu 12,000 toka katika kila kabila katika makabila kumi na mbili ya Israeli kwa ujumla wa 144,000. Hata yatatimizwa kwa majaliwa maalumu ya Mungu ambapo baadhi ya wana wa Ibrahimu, ambao Mungu aliwapaenda, wataokolewa. Mungu aliikumbuka ahadi aliyoifanya kwa Ibrahimu, hivyo ili kuitimiza ahadi hii, sasa ameiruhusu injili ya maji na Roho kuenezwa sio tu kwa wamataifa, bali pia kwa watu wa Israeli, ambao ni wana wa kimwili wa Ibrahimu. 
Kwa hiyo, Mungu ameazimia kwamba kwa kupitia dhiki ya nyakati za mwisho na kwa kupitia mashahidi wawili ambao Mungu atawainua kipekee kabisa kabisa kwa ajili ya Waisraeli, basi hapo ndipo Waisraeli watakapofikia hatua ya kumwamini Yesu Kristo, ambaye walimtesa na kumsulubisha, ndipo watatambua kwa hakika kuwa ni Mwokozi wao wa kweli. Waisraeli wamefanyika kuwa wapokeaji wa upendo maalumu wa Mungu kwa kupitia Mungu na imani ya Ibrahimu. 
Mungu ameamua kwamba atawakomboa watu 12,000 toka katika kila kabila ya Israeli toka katika dhambi zao na maangamizi, na kwa sababu hiyo amewawekea muhuri ya Mungu kwa kupitia malaika wake. Hivyo, watu 144,000 kati ya watu wa Israeli wamepokea alama inayowaonyesha kuwa wamefanyika kuwa watu wa Mungu. Idadi hii inagawanyika sawa miongoni mwa kabila kumi na mbili za Israeli, hii ni kwa sababu upendo wa Mungu kwa Waisraeli haupo katika misingi ya upendeleo kwa kabila fulani, bali anawavika wote kwa neema ile ile inayowafanya kuwa watu wake. Ingawa kwa baadhi ya nyakati watu huruhusu hisia zao kutawala hukumu na maamuzi yao, ukweli ni kuwa Mungu hutenda katika mambo haya yote kwa haki kamilifu na usawa. 
Baada ya kuwawekea muhuri wa wokovu watu 144,000 wa Israeli, basi hapo ndipo Mungu atakapoyamimina mapigo makuu hapa duniani. Mungu amefanya jumla ya Waisraeli 144,000 kuwa watu wake, watu 12,000 toka katika makabila kumi na mbili ya Israeli—yaani kuanzia kabila la Yuda, Rubeni, Gadi, Asheri, Naftali, Manase, Simioni, Lawi, Isakari, Zabuloni, Yusufu, na Benyamini. Mungu amefanya hili kuitunza ahadi aliyomwapia Ibrahimu na wana wake kwamba atakuwa Mungu wao. 
Hivyo, Mungu ameamua kuwaokoa watu 144,000 wa Israeli. Hii namba 14 kama inavyoonekana katika Mathayo 1:17 ina maana maalumu kwetu, inatueleza kwamba Mungu ataianza kazi yake mpya miongoni mwa Waisraeli. Namba hii inajumuisha mapenzi ya Mungu kwamba sasa ataihitimisha historia ya ulimwengu wa kwanza hapa duniani na kisha kuwaruhusu Waisraeli waliookolewa kuishi katika Mbingu na Nchi Mpya.
Tunapoangalia mtiririko wa ukoo toka kwa Ibrahimu hadi kwa Yesu Kristo, tunaweza kuona kwamba kuanzia Ibrahimu hadi Daudi kuna vizazi 14, na kutoka Dauti hadi wakati wa kuchukuliwa utumwamini Babeli kuna vizazi vingine 14, na toka kuchukuliwa utumwani Babeli hadi kuzaliwa kwa Kristo kuna vizazi vingine 14. Kwa maneno mengine, tunaweza kuona kwamba Mungu anaanza kazi mpya kila baada ya vizazi 14. Mungu amewatia muhuri Waisraeli 144,000 kwa mapenzi yake kwamba atawafanya waishi maisha mapya, si katika ulimwengu wa sasa, bali katika Ufalme wa Mungu. Kama inavyoweza kuonekana, Mungu ni mwaminifu anayezitimiza ahadi zake alizowahi kumwahidi mwanadamu.